

Lugha Nyingine
Biashara ya nje ya Shenzhen yaongezeka kwa asilimia zaidi ya 10 mwezi Machi
Picha iliyopigwa tarehe 23 Julai 2024 ikionyesha mwonekano wa Qianhai mjini Shenzhen, Mkoani Guangdong, kusini mwa China. (Picha na Tong Yanlong/Xinhua)
SHENZHEN – Mji wa kisasa wa kusini mwa China Shenzhen umeshuhudia thamani ya biashara yake ya nje ikifikia yuan zaidi ya bilioni 387.05 (dola za Kimarekani kama bilioni 53.7) mwezi Machi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.3 kuliko mwaka jana wakati kama huo, takwimu za forodha zilizotolewa jana Jumanne zinaonesha.
Katika mwezi huo wa Machi, uuzaji bidhaa nje wa mji huo yaliongezeka kwa kiasi kikubwa, yakifikia yuan bilioni 218.53, ikiongezeka kwa asilimia 8.8 kuliko mwaka jana wakati kama huo, wakati huohuo uagizaji bidhaa kutoka nje pia uliongezeka kwa asilimia 17.2 kufikia yuan bilioni 168.52, kwa mujibu wa Forodha ya Shenzhen.
Maafisa wa forodha wa mji huo wamesema kuwa, Shenzhen imeonyesha uhimilivu mkubwa katika biashara ya nje licha ya kukabiliwa na changamoto za nje zinazoongezeka na msingi wa juu kutoka mwaka uliopita.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa, jumla ya biashara ya nje ya mji huo ilifikia yuan bilioni 990.1 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, huku mauzo ya nje yakifikia yuan bilioni 585.5 na uagizaji bidhaa nje ukifikia jumla ya yuan bilioni 404.6. Licha ya kushuka kwa asilimia 8.7 kwa mauzo ya nje katika robo ya kwanza, uagizaji bidhaa nje ulikua kwa asilimia 7.1kuliko mwaka jana wakati kama huo.
Kampuni binafsi zimeendelea kuwa uti wa mgongo wa biashara ya nje ya Shenzhen. Takwimu zinaonesha kuwa katika Mwezi huo wa Machi, kampuni hizo binafsi zilichukua asilimia 69.6 ya jumla ya biashara ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa ya Shenzhen, ikifikia yuan bilioni 269.4, ongezeko la asilimia 13.8 kuliko kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Kampuni zinazowekezwa na mtaji wa kigeni pia zimerekodi ukuaji wa asilimia 9.3 wa biashara ya nje kuliko mwaka jana wakati kama huo, zikifikia yuan bilioni 102.17.
Biashara kati ya Shenzhen na wenzi wake 10 wakuu zote zimeongezeka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma